By Fikra Pevu
http://www.fikrapevu.com/muhimbili-yazidiwa-na-wagonjwa-wa-figo/ HOSPITALI ya Taifa ya Muhimbili, inapokea takribani wagonjwa 30 kwa siku kwa ajili ya kuchujwa damu kutokana na matatizo ya figo, hali inayosababisha Hospitali hiyo kukabiliwa na uhaba wa mashine hizo, kufuatia hospitali hiyo kuwa na mashine 17 tu. Mkurugenzi wa Huduma za uuguzi katika hospitali hiyo, Agnes Mtawa, ameiambia FikraPevu kuwa tatizo hilo limewafanya kushindwa kuhudumia wagonjwa wanaofika hospitalini hapo kwa wakati, na idadi ya wagonjwa wenye kuhitaji huduma hiyo imekuwa ikizidi kila siku. Aidha, amesema kwa sasa kitengo hicho kimepokea msaada wa mashine ya kusafisha damu kutoka ubalozi wa India, mashine ambayo inathamani ya zaidi ya shilingi milioni kumi za Tanzania. Amesema licha ya kuwepo kwa tatizo hilo, kitengo hicho kinakabiliwa na matatizo lukuki ikiwemo uhaba mkubwa wa madaktari bingwa wa magonjwa ya figo ambapo kwa sasa wapo madaktari saba tu huku wengine watatu wakiwa wapo nje ya nchi kwa ajili ya kupata elimu zaidi na kufanya kazi kwa shida. Tafiti mbalimbali zinaonyesha kuwa wataalamu wa afya wanasema kuwa zipo sababu kadhaa zinazosababisha maradhi katika figo kwa binadamu ikiwamo matumizi mabaya ya dawa hususani watu wanaotumia sawa za kupunguza maumivu, dawa za kienyeji, baadhi ya dawa za Kichina, uvutaji wa sigara na unywaji wa pombe kupita kiasi, licha ya kiungo hicho kuwa miongoni mwa viungo muhimu katika mfumo wa utendaji kazi wa mwili wa binadamu. - See more at: http://www.fikrapevu.com/muhimbili-yazidiwa-na-wagonjwa-wa-figo/#sthash.XGksozGR.dpuf
2 Comments
|
AuthorNephrology Society of Tanzania ArchivesCategories |